Skip to main content

BILIONI 57 KUTUMIKA KUJENGA KITUO CHA MAFUNZO YA ANGA NIT


Serikali imewekeza  jumla ya shilingi Bilioni 57 kwa ajili ya unjenzi wa   kituo cha umahiri cha Mafunzo ya Anga katika chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT )kilichopo Mabibo jijini Dar e salaam.


Hayo yamesema na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa leo Disemba 19,2025 wakati akizungumza kwenye mahafali yaliyofanyika chuoni hapo ambapo amesema kuwa 
Serikali imewekeza fedha nyingi katika kununua vifaa pamoja kujenga majengo ya kisasa ili watoto wa kitanzania wapate elimu iliyobora na kwa gharama nafuu, kwani ukienda nje ya nchi mafunzo haya hupatikana kwa gharama kubwa hivyo watanzania wengi watashindwa kusoma.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Mhandisi Prosper Mgaya amesema kuwa jumla ya wanafunzi 100 wameshaitimu katika chuo hicho katika fani ya Urubani, Wahudumu ndani ya ndege  na Wahandisi wa Matengenezo ya Ndege.


‘’ Baada ya kuanzisha masomo haya vijana wengi wamejiunga na chuo chetu katika fani za  Matengenezo ya Ndege,Wahudumu wa ndani ya Ndege na Urubani ‘’


Naye Mwenyekiti wa Bodi wa chuo hicho Prof. Ulingeta Bamba amasema kuwa elimu inayotolewa katika chuo hicho ni  Elimu inayokubalika kimataifa hivyo amewakaribisha vijana  kupata elimu katika chuo hicho

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI