Skip to main content

DKT. NCHIMBI KUZINDUA JENGO LA VIONGOZI MASHUHURI UWANJA WA NDEGE (JNIA)


Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania  Mhe.Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi anatarajiwa kuzindua Jengo Maalumu la Viongozi mashuhuri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Julius nyerere Dar es salaam ambapo jengo hilo litatumika na viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame mbarawa Amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza Miradi ya usafiri na usafirishaji kupitia  Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini ukiwemo Uwanja wa ndege wa Kimataifa cha Msalato Dodoma. Sumbawanga, Tabora, Manyara, KIA ,Shinyanga,Tanga  Iringa, na Songwe.

Katika kuhakikisha kuwa Shughuli ya utalii,biashara na kilimo zinaendelea kuimarishwa na kuleta tija kwa Taifa Wizara ya Uchukuzi kupitia Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) inaendelea na Hatua yakinifu na usanifu wa kina Kwa Viwanja vipya vya ndege vya Serengeti, Kagera na njombe huku Mara baada ya kukamilika upembuzi huo serikali itaweka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi hiyo Mitatu.


"Serikali imeendelea kuboresha Kampuni ya Ndege ya (ATCL) kwa kuongeza idadi ya ndege za Masafa ya kati na Marefu ili kuongeza wigo wa mtandao wake wa safari za kanda na kimataifa hivyo itafungua nchi katika kukudha Biashara na Uchumi.


Aidha Kwa sasa jengo mashuhuri la viongozi lililotekelezwa kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julias nyerere ambapo utekelezaji wake umekamilika.


Nitoe wito Kwa wananchi wote wa Mkoa wa  Dar es alaam kushiriki kwenye uzinduzi wa jengo hilo la viongozi wa kimataifa na wakuu wa nchi kwani jengo hilo ni la kisasa linatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16  na Makamu wa rais Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Mwaka huu kwenye uwanja wa kimataifa Julius nyerere"  Amesema Mbarawa".


Hata hivyo jengo hilo la kisasa lenye ghorofa moja linajumuisha kumbi tano za viongozi wa kitaifa zikiwemo kumbi mbili maalumu za mikutano, na migahawa.


Vilevile jengo hilo limefungwa mifumo ya kisasa ya umeme, Maji Tehama na vioyozi pia mradi huo ulikamilika Mwezi Oktoba 31 na kutekelezwa na mkandarasi CRJE chini ya usimamizi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania(TAA)huku kupitia mradi huo ulizalisha ajira rasmi na zisizo rasmi kwa Wazawa Takribani 1100,na kutoa kandarasi ununuzi, na usambazaji wa vifaa vya ujenzi vinavopatikana hapa nchini zikiwemo Saruji, Tofari, kokoto na Nondo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Matengenezo Focus Kadeghe ameongeza kuwa jengo hilo ni Mahususi kwa  kuhudumia Viongozi Mashuhuri ambapo Gharama za matengenezo na marekebisho ya viwanja vyote  Nchini vilivyotekelezwa ni Shilingi Trioni Mbili.


Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI