DKT. KIJAJI AONGOZA KIKAO CHA KUISUKA SEKRETARIETI YA BARAZA LA 14 LA USIMAMIZI UTEKELEZAJI MKATABA WA LUSAKA KENYA



Rais wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameongoza Kikao cha 14 cha Baraza la Usimamizi wa Utekelezaji wa Mkataba wa Lusaka unaohusika na kupambana na ujangili wa wanyamapori na misitu unaovuka mipaka ya nchi, Jijini Nairobi Kenya. 


Kikao hicho kinachozikutanisha  nchi wanachama wa Mkataba huo ikiwemo Kenya, Tanzania, Congo Brazavile, Zambia na Liberia kimefanyika hii leo Mei 20,2026 Jijini Nairobi Nchini Kenya. 


Kikao hicho kinatokana na maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha 14 cha Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka kilichofanyika Mwezi Mei, 2025 Jijini Arusha Tanzania. Miongoni mwa maazimio ya kikao kilichotangulia ni pamoja na kufanya maboresho ya utendaji na muundo wa Sekretariati ya Mkataba huo.  


Kikao cha hicho leo, kimepitia taarifa za utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichopita na taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Secretariati ya Mkataba kwa kipindi cha kuanzia Mei 2025 hadi Aprili 2026. Lengo ni kuendelea kuimarisha utendaji wa Secretariat ili kukabiliana na uhalifu wa wanyamapori na misitu unaovuka mipaka (transnational crime) katika nchi wanachama kwa ufanisi.


Katika kikao hicho, Dkt. Kijaji ameambatana na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Alexander Lobora, Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili Bw. Ezekiel Goboro pamoja na watendaji wa Wizara na Taasisi za Uhifadhi ikiwemo (NCAA, TANAPA na TFS 





Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI