RAIS TUCTA AUPONGEZA UONGOZI JOWUTA KWA KUENDELEA KUUNGANISHA WANACHAMA WAKE
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya ameupongeza uongozi wa Chama cha Wafanyakazi Wanahabari Tanzania (JOWUTA) kwa namna ambavyo unajitahidi kuwaleta pamoja Wanahabari na wanachama wake.
Nyamhokya ameitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kuhusu fidia kwa wafanyakazi (WCF)kwa wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanaofanya Kazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA), yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Mei 25, 2026.
Amesema suala la kuwajengea uwezo wanachama ni moja ya nyenzo muhimu kwa uhai wa chama chochote cha wafanyakazi na ni muhimu Wafanyakazi wawe na uelewa wa kutosha kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maisha yao ya kila siku na jamii inayowazunguka.
Amewataka Wanachama wa JOWUTA kuwa na Umoja na Mshikamano kwani ndio nguzo kuu na uimara wa Chama chochote chenye malengo ya kunufaika.
Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano na WCF kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wanahabari kuhusu haki, mafao na taratibu za fidia kwa wafanyakazi ili waweze kuripoti masuala hayo kwa usahihi kwa umma.





Comments
Post a Comment