KAIMU MENEJA WA TARURA NA FUNDI SANIFU NYASA WATIWA HATIANI KWA RUSHWA.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, imewafikisha mahakamani watumishi wawili wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Nyasa, akiwemo Kaimu Meneja wa TARURA wilayani humo, kwa makosa mbalimbali ya rushwa, yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka na kughushi nyaraka.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Arterio Kawonga, amesema TAKUKURU Wilaya ya Nyasa ilifanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kuwafikisha watuhumiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyasa katika shauri la uhujumu uchumi namba 5463/2026.
Amesema mahakama iliwatia hatiani watuhumiwa hao ambao ni Bw. Thomas Emilyo Kitusi, Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Nyasa, pamoja na Bw. Magela Benedict Mteleke, Fundi Sanifu wa Ujenzi katika wilaya hiyo.
Mahakama imeelekeza kurejeshwa kwa fedha zote kiasi cha shilingi 9,072,126, ambazo ni fedha za mradi wa UVIKO-19, katika akaunti ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Comments
Post a Comment