Posts

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mhe. Suzan Kaganda anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe pamoja na Balozi Mhe. Dkt. Habib Kambanga anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Machi 2025. Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa na imani waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliwakilisha Taifa kwenye nchi hizo. Aidha amewasihi kulinda na kutetea maslahi ya Taifa. Makamu wa Rais amewasisitiza Mabalozi hao kuwa na takwimu za msingi kuhusu maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania ili kuwa na uwakilishi mzuri katika maeneo yao hususani katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. Pia amewataka kufanya jitihada za makusudi kuzifahamu vema nchi wanazokwenda kuiwakilisha Tanzania ili kuweza kujifunza misingi ya ukuzaji wa uchumi wao na kuhamish...

PICHA: RAIS SAMIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI 8

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi 8 wanaowakilisha nchi zao Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

MIRADI MIKUBWA ILIYOPEWA LESENI IANZE UTEKELEZAJI

Image
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameagiza Miradi Mikubwa na ya Kati ya madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla na kutimiza azma ya Serikali kutoa leseni hizo. Amesema hayo, leo Machi 28, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kukutana na makundi yote yayojihusisha na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini. Waziri Mavunde amesema Serikali inataka kuhakikisha kuwa Miradi yote ya Uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa Serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa Sekta binafsi kuchukua hatua kwa upande wao. “S...

PICHA: WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHI ZA ZIMBABWE NA RWANDA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 28, 2025 amefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Habib Galus Kambanga (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Dkt. Suzan Kaganda (kulia), kwenye Ofisi ndogo  ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image

WATUMISHI WA NCAA WAPANDA MITI 1,000 NA MINGINE 10,000 WAGAIWA WANANCHI

Image
Na Mwandishi wetu, Karatu -Arusha Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) leo tarehe 28 machi, 2025 wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda tarehe 15 machi, 2025 kwa lengo la kutunza mazingira na kuboresha mandhari ya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii hapa nchini.  Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti lilofanyika ofisi za NCAA Karatu, Afisa Uhifadhi Mkuu anayesimamia sehemu ya Usimamizi wa wanyamapori na utafiti Lohi Zakaria amesema lengo la zoezi la upandaji miti kwa watumishi ni kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kutunza mazingira. “NCAA leo tumetekeleza maagizo yaliyotolewa na mkuu wa Mkoa wa Arusha kupanda miti, siku ya leo pekee tumepanda miche ya miti 1,000, tunaungana na serikali kuhakikisha kuwa tunakabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi hasa swala la hewa ukaa ambalo dunia nzima kwa sasa linapambana nao” Alisema L...

DKT. KAZUNGU AKUTANA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI

Image
-Wazungumzia jinsi Mfuko wa Uwekezaji Denrmark (IFU) utakavyosaidia kuendeleza Sekta ya Nishati nchini* -Dkt. Kazungu akaribisha uwekezaji Rumakali, Ruhudji na miradi iliyopo katika Mpango Mahsusi wa Taifa wa Nishati (2025-2030)* -Denmark yaahidi kuendeleza ushirikiano* Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Jesper Kammersgaard na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Denmark (IFU) Bw. Theo Ib Larsen. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma tarehe 27 Machi, 2025, Mhe. Kammersgaard pamoja na Larsen walikuwa na lengo la kueleza kuhusu Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Denmark ulioanzishwa mwaka 1967 ili kusaidia maendeleo katika nchi zinazoendelea kwa kutoa mitaji kwa kampuni zinazotaka kuwekeza katika masoko yanayoibukia barani Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na sehemu za Ulaya. Viongozi hao wameeleza kuwa IFU inaweza kutoa msaada wa kifedha na kiufundi katika eneo l...