MBUNGE NGASSA AWAHIMIIZA WANANCHI KILIMA PAMBA
Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa ametoa wito kwa wananchi wa jimboni kwake kulima pamba kwa wingi kwani zao hilo ni muhimu kwa maendeleo yao.
Mh.Ngassa ameyasema hayo Julai 16,2024 wakati akizungumza na wananchi alipokuwa kwenye ziara yake ya kutoa mrejesho mara baada ya kutoka kwenye Bunge la bajeti.
"Wana Igunga tuendelee kulima pamba kwa wingi,kwani zao la pamba ni dhahabu nyeupe"amesema Mh.Ngassa
Mh Ngassa ameendelea na Ziara Jimboni huku akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Wananchi pamoja na Kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti kwa Wananchi,Kuona Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Aidha Mh.Ngassa ameendelea Kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwenye maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi,kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 pamoja na Kusikiliza Kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Comments
Post a Comment