HESLB,TRA WABADILISHANA HATI ZA USHIRIKIANO

 

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Septemba 13,2024 Wamebadilishana za ushiriakiano baina yao kwa lengo la kuboresha huduma kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa Hafla hiyo fupi ya kubadilishana hati ya ushirikiano na wadau wa kimkakati,Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bill Kiwia amesema TRA ina jukumu la kuwatambua watu waliokatika Sekta mbalimbali hivyo ni furs adhimu kwetu kushirikiana nao kimkakati.

Kiwia Amesema kuwa kuna malengo makuu mawili ambayo yamewafanya kushirikiana na TRA ambalo lengo lake ni kuweza kuwafikia wanufaika wote ambao wana kipato na kuwatafuta hasa kwenye sekta zisizo rasmi pamoja na kuwafikia Watanzania kwa ujumla kwa lengo la kuboresha huduma zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRA Yusuph Mwenda ameipongeza HESLB kwa kazi kubwa ya kutoa mikopo ambayo imekuwa na wanufaika wengi na hii ni kwa sababu ya watanzania wanaolipa kodi ambayo inaenda kuwasaidia watoto na ndugu zao ambao wanasoma.

Aidha amewapongeza Watanzania ambao wanaolipa kodi kwani kodi zao zinatumika vizuri na ndizo zinazofanikisha maendeleo mbalimbali ndani ya Nchi.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI