MWENYEKITI NLD AWATAKA WANACHAMA KUMUUNGA MKONO DOYO

Wanachama wa Chama cha National League for Democracy (NLD), wameombwa kumuunga mkono Katibu Mkuu  Doyo Hassan Doyo kwani ni mtu muadilifu na mtendaji mzuri wa kazi ili kuleta mabadiliko na maendeleo ndani ya chama hicho

 Hayo yamesemwa Septemba 11, 2024  na Mwenyekiti wa Chama hicho Mfaume Khamis Hassan wakati alipokuwa akizungumza na Wanachama na kusema kuwa ili kuleta mabadiliko na Maendeleo kwenye chama ni muhimu kumuunga mkono na kusimama nae kwa pamoja

 

"Hakuna chama chochote kinachoweza kumkataa mtu kama Doyo, mtu mwenye historia ya utendaji bora katika siasa za nchi hii."  Amesema Hassan

 Mwenyekiti wa NLD, Katibu Mkuu wa Chama hicho walifanya kikao cha ndani na baadhi ya wanachama wa chama hicho upande wa Zanzibar, ambapo wote kwa pamoja walitoa mwito wa kuimarisha ujenzi wa chama na ushirikiano kati ya wanachama wa NLD kutoka Bara na Zanzibar.

Katika ziara hiyo, Doyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka upande wa Bara na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho upande wa Zanzibar, akiwemo Mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa, Mhe. Mfaume Khamis Hassan.

Kwa upande wake, Mhe. Doyo aliwashukuru wanachama wa NLD kwa utayari wao wa kufanya kazi naye, na akawahakikishia kwamba atafanya mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupi. 

 Hata hivyo Doyo ameahidi kukifanya chama hicho kuwa miongoni mwa vyama shindani katika chaguzi zijazo.  

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI