NLD KUENDESHA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA AMANI
Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba, Chama cha National League for Democracy (NLD), Kimesema kuwa kitaendesha Kampeni za Chama hicho Kwa njia ya amani.
Akizungumza kwenye Kikao Cha ndani na Viongozi wa Chama hicho kutoka Chaani Zanzibar,Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama hicho, Ahmed Hamad,amewataka viongozi wa NLD Zanzibar kuongozwa na busara wanapoeneza sera na itikadi ya chama cha NLD, Alisisitiza.
"Chama cha NLD kitaendesha kampeni za busara, kuepuka uchochezi, udanganyifu, au vurugu, na badala yake tutaweka msisitizo kwenye hoja na sera, kwani NLD ina sera nzuri kuliko chama chochote nchini."
Aidha Hamad aliwahimiza viongozi wa NLD kuhakikisha wanajenga mahusiano bora na wananchi wa ngazi za chini huku akitaka Viongozi hao kutatua Changamoto za wananchi kupitia Sera za Chama hicho.
Chama cha NLD kipo kwenye Ziara ya siku nne visiwani Zanzibar, inayoongozwa na Katibu Mkuu wa NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, Ziara hiyo inashirikisha viongozi wakuu wa chama hicho, na inahusisha ujenzi na kuimarisha chama kwenye ngazi za uongozi.
.jpg)
Comments
Post a Comment