MAZINGIRA BORA YA ELIMU YAIMARISHWA MBINGA, SHULE YA MASHAUJAA LITEMBO YAZINDULIWA

 


Ili kuwawezesha wanafunzi kuingia kikamilifu kwenye ushindani wa maarifa na fikra, ni muhimu kuwaandalia mazingira bora ya kujifunzia pamoja na huduma muhimu zinazochochea upatikanaji wa elimu yenye ubora. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imejenga Shule ya Sekondari Mashujaa Litembo iliyopo Kata ya Litembo, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kwa gharama ya shilingi milioni 701,952,701.


Akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi tarehe 26 Aprili 2026 wakati wa uzinduzi wa shule hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, amesisitiza kuwa jukumu la kuwaandaa watoto kwa ajili ya ushindani wa kifikra ni la pamoja kati ya serikali na wazazi. Ameeleza kuwa mazingira bora ya kujifunzia ni msingi muhimu utakaowawezesha wanafunzi kupata maarifa sahihi na kufikia malengo yao kielimu.


Aidha, Mhe. Makori amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kutoa fedha zinazowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa shule hiyo, hatua inayochangia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.


Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbinga, ndugu Aly Simba, amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao. Amesisitiza kuwa utunzaji wa miradi hiyo utahakikisha inaendelea kutoa manufaa kwa muda mrefu kwa jamii nzima.




Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI