TASACO YAPONGEZWA KWA KUWASAIDIA WENYE UHITAJI
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mwanaisha Ally ameipongeza
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Samaritan Community Organizationin (TASACO) kwa kuwawezesha na kuwasaidia mahitaji ya vifaaa vya shule kwa watoto wenye uhitaji.
Bi Mwanaisha ameyasema hayo leo Julai 24 ,2026 Kivule Wilayani Ilala Jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Kikundi vya Ujasiriamali
Kivule (Kivule Samaritan Unity).
Ameongeza kuwa kwa kitendo cha kusaidia watoto yatima na walio na wazazi wasio na uwezo ni kuisaidia jamii kuondokana na Umasikini sambamba na kupata vijana ambao baadae watakwenda kusaidia Maendeleo Nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TaSaCo Paul Chegere amesema kuwa Uzinduzi wa Kivule Samaritan Unity ni kiashiria kizuri cha ukamilifu wa maono ya Shirika hilo ambayo ni kuwezesha wananchi kichumi na kupitia vikundi vilivyoanzishwa wataweza kukopeshana kwa masharti nafuu na muda mzuri wa marejesho ambapo itasaidia kukuza mitaji na kipato kuongezeka.







Comments
Post a Comment