Posts

MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT. NCHIMBI, ATEMBELEA UWANJA WA AFCON ARUSHA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha, utakaotumika katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027), unaojengwa Jijini Arusha.   Makamu wa Rais amepongeza maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, ambapo amesema ni faraja kuona ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa ili kuvutia michuano hiyo kufanyika nchini Tanzania, inatakelezwa kikamilifu. Amemshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kutoa fedha ili kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati.   Aidha, Makamu wa Rais ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mkoa wa Arusha, Wakandarasi na Mshauri Elekezi kwa kazi kubwa waliyofanya katika Uwanja huo.   Makamu wa Rais amewataka Viongozi wa Wizara pamoja na Mkoa wa Arusha kusimamia vema agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha barabara zinazotumika katika kufika uwanjan...

TASACO YAPONGEZWA KWA KUWASAIDIA WENYE UHITAJI

Image
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mwanaisha Ally ameipongeza  Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Samaritan Community Organizationin (TASACO) kwa kuwawezesha na kuwasaidia mahitaji ya vifaaa vya shule kwa watoto wenye uhitaji. Bi Mwanaisha ameyasema hayo leo Julai 24 ,2026 Kivule Wilayani Ilala Jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi wa Umoja wa Kikundi vya Ujasiriamali  Kivule (Kivule Samaritan Unity). Ameongeza kuwa kwa kitendo cha kusaidia watoto yatima na walio na wazazi wasio na uwezo ni kuisaidia jamii kuondokana na Umasikini sambamba na kupata vijana ambao baadae watakwenda kusaidia Maendeleo Nchini. Kwa upande wake Mkurugenzi wa TaSaCo Paul Chegere amesema kuwa Uzinduzi wa Kivule Samaritan Unity ni kiashiria kizuri cha ukamilifu wa maono ya Shirika hilo ambayo ni kuwezesha wananchi kichumi na kupitia vikundi vilivyoanzishwa wataweza kukopeshana kwa masharti nafuu na muda mzuri wa marejesho ambapo itasaidia kukuza mitaji na kipato kuongez...

UTU WA TAIFA HUPIMWA KWA NAMNA LINAVYOWAJALI WAZEE WAKE – NAIBU WAZIRI MAHUNDI

Image
  Na Jackline Minja WMJWM Bukoba, Kagera Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha wazee nchini wanapata huduma bora na stahiki kwa kuimarisha makazi ya wazee, huduma za afya pamoja na mazingira salama yanayolinda utu na heshima yao. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipofanya ziara ya kutembelea Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima yaliyopo Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma, kusikiliza changamoto pamoja na kuhimiza maboresho ya ustawi wa wazee.  Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali itaendelea kuimarisha huduma za ustawi wa jamii kwa wazee ili kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama, yenye heshima na yanayokidhi mahitaji yao ya msingi, ikiwemo huduma za afya, lishe, malazi na huduma za kijamii kwani Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee katika kujenga Taifa, hivyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ku...

WACHIMBAJI WADOGO WAISHUKURU SERIKALI KWA USAMBAZAJI WA UMEME MIGODINI

Image
Wachimbaji wadogo wa madini wilayani Nyang'hwale, mkoani Geita, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika upatikanaji wa nishati ya umeme kwenye maeneo ya migodi, hatua inayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji. Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alipozindua mradi wa kuzalisha nishati ya umeme wenye uwezo wa KVA 500 kwenye Mgodi wa wachimbaji wadogo katika eneo la Igalula, wilayani Nyang'hwale. Mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 426 na ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya nishati katika maeneo ya uchimbaji wa madini. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Mavunde amesema Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na uzalishaji katika sekta ya madini kwa kusambaza umeme kwenye migodi ya wachimbaji ...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

TUNDUMA YAUNGANA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

Image
Watendaji wa kata na mitaa, wenyeviti, mabalozi wa nyumba kumi pamoja na viongozi wa dini zote wa Mji wa Tunduma wametakiwa kuendelea kushirikiana katika kupambana na vitendo vya ulawiti, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia ili kulinda usalama wa watoto na jamii kwa ujumla. Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 21 Julai 2026, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mji wa Tunduma, Mrakibu wa Polisi Daud Nalimi, akiwa pamoja na Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Momba, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Frida, aliwataka viongozi hao kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi, hususan Polisi Kata, ili kuimarisha ulinzi wa jamii, kuzuia uhalifu na kuhakikisha wahalifu wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wanachukuliwa hatua za kisheria. Kwa upande mkuu wa Polisi jamii wilaya ya Momba amewahimiza viongozi hao kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, kuripoti matukio ya ukatili kwa wakati na kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kutokomeza kabisa vitendo vya ulawiti, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia k...

JESHI LA POLISI MBEYA LAWASHUKURU WADAU NA WANANCHI KWA USHIRIKIANO

Image
Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia vifaa vya kielektroniki pamoja na mifumo mbalimbali ya kidigitali, wananchi na wadau Mkoani humo wapongezwa kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzuia na kutokomeza uhalifu. Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wilbert Siwa Julai 21, 2026 wakati akipokea msaada wa "Computer" iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Ilemi kwa ajili ya kusaidia kazi za Polisi Jamii Wilaya ya Mbeya. "Msaada huu umekuja wakati muafaka ambapo Jeshi la Polisi nchini limejikita katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya kidigitali katika utendaji wake wa kazi, hivyo vifaa hivi vitasaidia kuongeza ufanisi na weledi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali" alisema Kaimu Kamanda Siwa. Aidha, Kaimu Kamanda Siwa amesema kuwa elimu inayotolewa na Polisi na Wakaguzi Kata kwa makundi mbalimbali imesaidia wananchi kujua wajibu wao na kuzaa matunda iki...