Posts

Showing posts from September, 2026

WAZIRI MKUU AKUTANA NA VIONGOZI WA MADEREVA, MGOMO WASITISHWA

Image
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Viongozi wamekubali kusitisha mgomo uliodumu kwa siku mbili, ili huduma za usafiri ziendelee kama kawaida huku Serikali ikiwa tayari kusikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva.

TIDO AWATAKA WAANDISHI KUPANUA WIGO WA HABARI

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Mshauri wa Rais katika Masuala ya Habari, Bw. Tido Mhando, amewataka Waandishi wa Habari kupanua wigo wa habari wanazoripoti kwa kuangazia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, badala ya kujikita zaidi katika michezo na burudani. Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Clouds Media Group waliokuwa wakishiriki mafunzo kwa siku tano kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba, 2026 kuhusu mchakato na taratibu za ithibati, Bw. Mhando amesema pamoja na umuhimu wa habari za michezo na burudani, vyombo vya habari vina wajibu wa kuibua na kuripoti masuala mengine yenye maslahi kwa Taifa. “Ni sawa kuzungumzia michezo, lakini isiwe wakati wote. Lazima sisi kama Waandishi wa Habari tuone na kuripoti mambo mengine yanayoendelea katika nchi yetu,” amesema Bw. Mhando. Amesema Waandishi wa Habari wa ndani wana haki na wajibu wa kuripoti matukio yanayotokea nchini kwa usahihi na kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, badala ya kuacha simulizi kuhusu Ta...

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO

Image
  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.  Sehemu ya wajumbe wa Management ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ************** Na. Mwandishi W...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Image
  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, imesema uchaguzi huo unafanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi za uongozi katika maeneo ya uchaguzi.   “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma,” ilisema taarifa hiyo.   Nafasi hiyo imetokea baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Deogratius John Ndejembi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Uteuzi wake ulifanyika tarehe 26 Agosti, 2026 na kuthibitishwa na Bunge tarehe 28 Agosti, 20...

TANZANIA YATOA WITO KWA DUNIA KUFANYA KWA VITENDO AHADI YA KUKABILI ATHARI ZA KUPANDA KWA KINA CHA BAHARI

Image
Tanzania imetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza kasi ya upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi, teknolojia na mifumo madhubuti ya tahadhari za mapema ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na athari zinazoongezeka za kupanda kwa kina cha bahari.   Akihutubia Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupanda kwa kina cha Bahari mjini New York, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amesema tatizo hilo si tishio la siku zijazo tena, bali tayari linaathiri maisha ya watu, uchumi na mifumo ya ikolojia duniani.   Kwa Tanzania, athari hizo ni kubwa kutokana na ukanda wake wa pwani ya Bahari ya Hindi, Zanzibar na visiwa vingine ambavyo vinategemewa na mamilioni ya watu kupitia uvuvi, utalii na biashara. Mmomonyoko wa fukwe, kuingia kwa maji ya chumvi katika vyanzo vya maji baridi na mafuriko vinatajwa kuwa miongoni mwa vitisho kwa wananchi, miundombinu na mafanikio ya maendeleo ya nchi.   Ma...

MAMA FATMA KARUME AFARIKI DUNIA

Image
  Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia leo, Septemba 21, 2026. Taarifa za kifo chake zimefika wakati akiwa nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Zanzibar. Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, ambaye aliiongoza Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Kifo chake ni msiba mkubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar. Taarifa zaidi kuhusu mazishi na ratiba nyingine za msiba zinatarajiwa kutolewa na Serikali. Mama Fatma Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 97.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MKUTANO WA AFYA MOJA NCHINI ITALIA

Image
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 19, 2026) kwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.   Mkutano huo utakaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma, Italia kuanzia Septemba 21–23, 2026 unalenga kuimarisha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) inayotambua uhusiano kati ya afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira, kwa lengo la kuhakikisha mifumo endelevu ya chakula na kilimo   Mkutano huo utahusisha viongozi wa nchi na Serikali, wakiwemo Marais kati ya watano hadi saba, Mawaziri kati ya 30 hadi 50, pamoja na wawakilishi wa taasisi za kikanda na kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, taasisi za utafiti na mashirika ya kimataifa.   Mambo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni Ujumuishaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) katika sera na uw...

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MTO NG’OMBE, AAGIZA TAKA ZIONDOLEWE HARAKA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mto Ng’ombe, Tandale jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya usafi wa mazingira na maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.   Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Waziri wa TAMISEMI pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ndejembi ameelekeza Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mto huo unasafishwa na taka zilizorundikana kandokando ya Mto Ng’ombe zinaondolewa haraka na mazingira yanaendelea kuwekwa katika hali ya usafi.   Amewaagiza Viongozi wa Halmshauri, kupitia maafisa mazingira na maafisa maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzingatia usafi na ukusanyaji wa taka. Amesema ni muhimu kwa Halmashauri kuweka miundombinu mizuri ya kukusanya taka na kuzichukua kwa wakati ili wananchi wasitupe taka hizo katika maeneo yas...

LOWASSA: MSHIKAMANO TANZANIA, MAREKANI UONGEZE FURSA ZA UWEKEZAJI

Image
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tan Communication Media Ltd, inayomiliki na kuendesha kituo cha redio cha Redio 5 cha jijini Arusha, Robert Lowassa, amesema mshikamano baina ya Marekani na Tanzania yaongeze fursa zaidi za uwekezaji nchini. Lowassa ameyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Msemaji na Afisa Habari wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Nice Cole ofisini kwake Arusha.   Amesema Marekani imekuwa mshirika muhimu kwa Tanzania katika maeneo mbalimbali, ikiwemo utalii, biashara, uwekezaji na miradi ya maendeleo.   Lowassa amesema ni matumaini yake kuwa mshikamano huo utaendelea kuwa imara zaidi ili kufungua fursa nyingi zaidi za uwekezaji na maendeleo kwa manufaa ya pande zote mbili.   Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TanMedia, Angela Maina, amekaribisha ushirikiano huo, akisema Arusha na Tanzania kwa ujumla vina nafasi kubwa ya kunufaika zaidi kupitia mafunzo kwa vijana na waandishi wa habari, pamoja na programu za kubadilishana uzoefu (excha...