Posts

Showing posts from August, 2026

CHAMA CHA WAZEE NGUZO YA MALEZI, UPATANISHI, UTUNZAJI MAADILI YA KIJAMII

Image
Na WMJJWM - DODOMA Serikali imewataka viongozi wa Chama cha Wazee Wanaume Tanzania (CCWWT) kuhakikisha chama hicho kinakuwa chombo muhimu cha malezi, upatanishi na utunzaji wa mila, desturi na maadili ya jamii  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, katika  Mkutano Chama cha Wazee Wanaume Tanzania (CCWWT) jijini Dodoma Agosti 29, 2026. Profesa Shemdoe  amesema wazee ni tunu na hazina ya Taifa kutokana na mchango wao katika malezi, makuzi na ujenzi wa jamii hivyo wana jukumu la kurithisha Hekima zao kwa Jamii.  Ameongeza pia, wazee wana nafasi kubwa ya ushauri Malezi na upatanishi wa migogoro katika jamii, hivyo wanapaswa kuwaunganisha wazee na kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo.  Aidha, Shemdoe amebainisha kwamba, Serikali inaendelea  kutunza wazee ambapo jumla ya wazee 229 ...

SPIKA ZUNGU APOKEA JINA LA MAKAMU WA RAIS MTEULE

Image
  Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) leo tarehe 28 Agosti 2026 amepokea jina la Makamu wa Rais Mteule lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi.  Jina hilo limewasilishwa kwa Mhe. Spika na Katibu wa Rais  Bal. Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brig. Jen. Nyamburi Mashauri kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.  Mapokezi ya Jina hilo yameshuhudiwa na Naibu Spika Mhe. Daniel Sillo(Mb) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari (Mb) pamoja na Katibu wa Bunge , Ndugu Baraka Leonard.

RAIS SAMIA AZINDUA RASMI KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA BWAWA LA JULIUS NYERERE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 leo, tarehe 22 Agosti 2026, katika eneo la mradi lililopo Rufiji, mkoani Pwani. Viongozi mbalimbali wameungana na Rais Samia katika uzinduzi huo, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Moustafa Madbouly; Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi; pamoja na viongozi wengine. Uzinduzi wa JNHPP ni kilele cha utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati uliotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huo umegharimu takribani shilingi trilioni 7.452, sawa na dola za Marekani bilioni 3.35. Ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025. JNHPP imeongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini na kuimarisha usalama wa nishati. Kwa sasa, u...

MHE.MAHUNDI AWATAKA VIJANA KUTUMIA MICHEZO KUPATA AJIRA

Image
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka  vijana kutumia michezo kama fursa ya kujipatia ajira na kujenga maisha yao, huku wakiepuka vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na ukatili wa kijinsia. Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu 13 za Kata ya Iwambi jijini Mbeya. Amesema michezo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuwaweka vijana pamoja, kuwajengea vipaji na kuimarisha amani na mshikamano katika jamii huku akiwataka wananchi wa Iwambi kuunda timu moja imara itakayowakilisha kata hiyo katika mashindano mbalimbali na kuitangaza Iwambi kupitia michezo. Aidha, amependekeza kuanzishwa kwa klabu ya mbio za pole (jogging) katika kata hiyo, akisema mazoezi ni muhimu katika kuimarisha afya na kusaidia jamii kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwani michezo inapaswa kuwa chombo cha kuimarisha upendo na mshikamano ndani na nje ya Kata ya Iwambi, huku akitoa wito wa kushirikiana ka...

WIZARA YA MADINI YAFUMUA SOKO LA MADINI LISILO RASMI DAR ES SALAAM NA KUKAMATA WAHUSIKA

Image
Wizara ya Madini imefanikiwa kufanya oparesheni maalumu ya kuwasaka wafadhili na wawezeshaji wa wanunuzi wa madini wanaofanya biashara hiyo nje ya mfumo wa masoko yaliyoidhinishwa na Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 9,2026 katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde amesema oparesheni hiyo ni utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa tarehe 27 Julai, 2026 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Amesema maelekezo hayo yalitolewa baada ya Serikali kukamata madini ya dhahabu yaliyokuwa yakitoroshwa nje ya nchi. “maagizo kwa kikosi kazi kuhakikisha kinawakamata wale wanaowafadhili watoroshwaji wa madini. Tulitaka kujua madini haya yaliyokamatwa mikoani yanaishia wapi na yanauzwa na nani,” alisema Waziri Mavunde. Waziri Mavunde amebainisha kuwa kupitia oparesheni hiyo, Wizara imefanikiwa kubaini kuwepo kwa soko la madini lisilo rasmi katika eneo la Mtaa wa Jamhuri, jijini Dar es Salaam, katika jengo moja la ghorofa tano. Ameeleza...

MHE. MAHUNDI ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWAKILISHI WA MWENYEKITI WA UWT TAIFA KATIKA ZIARA YA KIKAZI CHUNYA

Image
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameshiriki mapokezi ya Mhe. Dkt. Catherine Canute aliyemwakilisha Mwenyekiti wa UWT Taifa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Chunya. Ziara hiyo imelenga kukagua uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/2030 na namna miradi ya maendeleo inavyotekelezwa katika wilaya hiyo. Akizungumza katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), pamoja na taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Mhe. Dkt. Catherine Canute amewapongeza viongozi wa Chama, wakiwemo wabunge na viongozi wa Serikali, kwa ushirikiano wao katika kusimamia na kuharakisha maendeleo ya Wilaya ya Chunya. Aidha, amempongeza Mhe. Mhandisi Maryp...

VIJANA TUJITOKEZE KUITETEA SERIKALI DHIDI YA UCHOCHEZI UNAOFANYWA MITANDAONI: ENG MARYPRISCA MAHUNDI.

Image
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Eng. Maryprisca Mahundi amewataka vijana kusimama kusimama imara kukemea Uchochezi na upotoshwaji  unaoenezwa mitandaoni  dhidi ya Serikali na kusimama imara kuitetea Serikali kwa hoja zenye nguvu. Eng.Mahundi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa UVCCM Tawi la Chuo Cha  ADEM Kampusi ya Mbeya katika mkutano maalumu wa Tawi la UVCCM chuoni hapo. "Tujitokeze kukemea Uchochezi dhidi ya serikali yetu unaoenezwa mitandaoni,tueleze mazuri ya serikali yetu kwa hoja" alisema Eng Mahundi. Aidha Naibu Waziri Mahundi ambaye pia ni Mbunge Viti Maalumu anayewakilisha Wanawake UWT Mkoa wa Mbeya kuwa mstari wa mbele kulinda amani na utulivu wa nchi jambo ambalo litachangia kuwa na fursa ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato na kujiinua kiuchumi. Amesema Vijana wanapaswa kutumia  vyema nguvu na Elimu yao  kwa kujiendeleza kiuchumi kwa kuwa Maendeleo ya nchi yanategemea zaidi Elimu na nguvu wa...

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA NANE NANE - DODOMA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuendelea kufanya usimamizi wa vyama vya ushirika na kutoa miongozo ya kitaalamu kwa vyama vyote nchini.   Makamu wa Rais ametoa wito huo, wakati wa Siku Maalum ya Ushirika katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane kwa mwaka 2026, yanayofanyika katika Viwanja vya John Malecela, Nzuguni mkoani Dodoma. Amesisitiza Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kuhakikisha linaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyama vya ushirika kwa lengo la kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya fedha, kuzuia ubadhirifu na kuongeza uwazi katika uendeshaji wa vyama hivyo.   Makamu wa Rais, amesema Ushirika wenye uadilifu ni muhimu sana katika kujenga imani kwa wanachama na kuvutia uwekezaji zaidi. Amesema kuimarika kwa ushirika kunategemea uwajibikaji, uaminifu na uadilifu wa wanachama, viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika.   Makamu wa Rais ...

MAANDALIZI YA UFUNGUZI WA LIGI YA TAIFA YA MPIRA WA WAVU YAPAMBA MOTO

Image
 Maandalizi ya ufunguzi wa Ligi ya Taifa ya Mpira wa Wavu yanaendelea katika Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam, leo Agosti 3, 2026, huku kila kitu kikiwa tayari kwa uzinduzi wa mashindano hayo. Mashabiki wanatarajiwa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kabla ya kushuhudia mchezo wa ufunguzi wa wanaume utakaowakutanisha Jeshi Stars dhidi ya Tanzania Prisons katika mtanange unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.