Posts

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MAZISHI YA MZEE EDWIN MTEI

Image
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 24, 2026, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya marehemu Mzee Edwin Mtei, yanayofanyika Tengeru, jijini Arusha. Mzee Edwin Mtei, ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia mwaka 1966 hadi 1974, alifariki dunia usiku wa Januari 19, 2026, jijini Arusha.

WATENDAJI WA UCHAGUZI PERAMIHO WATAKIWA KUVISHIRIKISHA VYAMA VYA SIASA

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe. Washiriki wa mafunzo  ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mwemyekiti wa Tume. Washiriki wa mafunzo  ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufung...

REA, EACOP ZAINGIA MAKUBALIANO KUPELEKA UMEME JAMII PEMBEZONI MWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA

Image
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) zimeingia makubaliano yaliyolenga kufikisha umeme katika vitongoji na jamii ambazo zimepitiwa na bomba hilo la mafuta kwa upande wa Tanzania. Mkataba huo wa ushirikiano ambao utatekelezwa kwa miaka mitano, umesainiwa leo Januari 23, 2026 Jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Guillaume Dulout. Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Saidy amesema kuwa makubaliano hayo yatahakikisha jamii zinazoishi pembezoni mwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Mkoa wa Kagera mpaka Mkoa wa Tanga zinafikiwa na kunufaika na mradi huo kwa kufikishiwa huduma ya umeme. Mhandisi Saidy ameongeza kuwa ushirikiano huo pamoja na manufaa mengine unalenga kuimarisha huduma za kijamii kama shule, vituo vya afya na miradi ya maji, pamoja na kuchochea matumizi ya umeme kwa shughuli za uzalishaji mali na...

KAMATI YA BUNGE YAKUTANA KUJADILI SERA YA MAMBO YA NJE

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imekutana kujadili utekelezaji na mwelekeo wa Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb.), kilichofanyika tarehe 23 Januari, 2026 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Kinyasi Millya (Mb.), amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa kwa ufanisi sambamba na mabadiliko ya mazingira ya kimataifa, ili kulinda na kukuza maslahi ya Taifa. Kikao hicho, kilichowakutanisha wajumbe wa Kamati hiyo na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kililenga kutathmini namna utekelezaji wa sera hiyo unavyoendelea kuimarisha maslahi ya Taifa katika nyanja z...

KAMATI YAPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI UBORESHWAJI HUDUMA ZA AFYA

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Dkt. Lembulung Lukumay ameipongeza Serikali kwa kuwekeza fedha katika ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa upatikanaji vifaa tiba.  Dkt. Lukumay ametoa pongezi hizo leo tarehe 23 Januari,2026 Jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya Muundo na Majukumu ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) iliyo chini Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu.  “Serikali imeongeza idadi ya madaktari wabobezi katika jitihada za kuboresha huduma za afya ikiwemo kuweka utaratibu mzuri wa kuendelea kuwezesha afua za UKIMWI kwa kutegemea fedha zetu za ndani ili kuendeleza upatikanaji wa dawa,” alieleza Dkt. Lukumay.  Aidha, amebainisha kuwa, wananchi hawana budi kuelezwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan katika uimarishaji wa huduma za afya, katika ngazi ya Zahanati, Vituo vya afya, hospitali za Wilaya na hospitali za Mi...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

WATENDAJI KITUO CHA UOKOZI MWANZA WATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA KWA SAA 24

Image
Na mwandishi wetu MWANZA Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu. Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza  Amesisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika. “Hii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi saa 24.” Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthubitisho wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia watanzania na kujali changamoto mbalimbali nchini.  “Kituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 kwenda Mwaka 2020, kilisimama baada ya wenzetu kujitoa, lakini Rais ...