SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUIMARISHA UTAYARI KUKABILIANA NA EL NINO
Na, mwandishi wetu - Dar es Salaam SERIKALI imezitaka taasisi mbalimbali nchini kufanyia kazi mapungufu na changamoto zilizobainika katika zoezi la kitaifa la uigaji wa dharura za mafuriko yanayohusishwa na mvua za El NiƱo ili kuimarisha utayari na uwezo wa kukabiliana na maafa kabla hayajatokea. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, wakati akifunga Zoezi la Kitaifa la Mezani la Uigaji wa Dharura kwa Taasisi Mbalimbali (SIMEX), lililofanyika kwa siku mbili Tanzania Bara. Amesema zoezi hilo limekuwa muhimu katika kupima mipango ya utayari wa kukabiliana na dharura kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi za chini, hususan katika uratibu wa sekta mbalimbali, majukumu ya kitaasisi, usimamizi wa taarifa na uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati. “Mapungufu na changamoto zilizobainishwa zisichukuliwe kuwa udhaifu, bali ziwe fursa muhimu za kuimarisha utayari wetu kabla maafa hal...