Posts

Showing posts from October, 2026

INEC YAWAPA NENO MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA KATA YA NONDE

Image
  Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika kata ya Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kutekeleza majukumu yao kwa weledi.   Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2026 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na watendaji hao alipotembelea mafunzo yao ya siku moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Nonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba,2026.   Jaji Mwambegele  amewasisitiza washiriki hao  kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.   Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo haya, washiriki hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki na weledi.   Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni miongoni mwa kata  kata 11 za Tanzania Bara ambazo ni Lugenge...

TUNDU LISSU HAJAGOMA KULA NA HAKUNA WAKILI ALIYEZUILIWA KUINGIA GEREZANI

Image
   

SERIKALI YALAANI UBAKAJI, YATOA WITO KWA WANANCHI KUTOKUINGILIA KESI ZA UKATILI

Image
Serikali imelaani vikali vitendo vya ubakaji na ukatili wa kijinsia vinavyosababisha waathirika kupata mimba, huku ikiwataka wazazi, ndugu na wananchi kwa ujumla kutokuingilia mchakato wa kisheria katika kesi zinazohusu ubakaji na ulawiti, ili kuhakikisha waathirika wanapata haki na wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, kuhusu kauli ya Serikali juu ya matukio ya ubakaji yanayoendelea na kusababisha waathirika kupata mimba, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha utekelezaji wa sheria zinazolinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, ikiwemo ubakaji na ulawiti. Katika majibu ya Serikali, imeelezwa kuwa kuanzia Januari hadi Desemba 2025, jumla ya makosa 7,219 ya ubakaji yaliripotiwa na kushughulikiwa, hatua inayoonesha umuhimu wa kuendelea kuimarisha mikakati ya kukabiliana na vitendo hivyo na kuhakikish...

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO OKTOBA 27,2026

Image
 

KAMANDA MULIRO AWATAKA MAAFISA USAFIRISHAJI KUDUMISHA USALAMA

Image
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Muliro J Muliro awataka Maafisa Usafirishaji kudumisha usalama wa nchi wakiwa katika majukumu yao ya Usafirishaji.  Kauli hiyo imetolewa Oktoba 22, 2026 alipokuwa akizungumza na Shirikisho la Madereva Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya 'ONGEA NA KAMANDA'.

TANESCO KUIWEZESHA KAMPUNI YA HWTZ MEGAWATI 200 KUTEKELEZA MRADI WA UZALISHAJI UMEME

Image
Waziri wa Nishati Dkt. Juma Homera amesema Shirika la umeme Tanzania TANESCO linatarajia kuingia makubaliano na muwekezaji kutoka Kampuni ya Hongwang Tanzania Holdings (HWTZ ) kutoka China kumpatia jumla ya Megawati 200, kwa ajili ya ujenzi wa Mradi mkubwa wa kuzalisha zaidi ya megawati 2,000 za umeme kwa kutumia makaa ya Mawe na nishati ya jua Mkoani Ruvuma. Akizungumza Oktoba 23, 2026 wakati wa ziara yake katika kongani ya viwanda inayojihusisha na uwekezaji wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji Umeme, Kiwanda cha Alminium pamoja na Chuma , Waziri Homera ametoa rai kwa TANESCO kuharakisha mchakato wa kuingia makubaliano ili mradi huo uanze kutekelezwa kwa haraka kwa maslahi mapana ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na maeneo jirani. Amesema Mradi huo unatakelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 7.8 ukitarajia kuzalisha zaidi ya megawati 2,000 za umeme ukipishana kidogo na Kituo cha kuzalisha umeme cha Julius Nyerere kinachozalisha jumla ya megawati 2115. ‘’ Tumeelezwa Mradi huu utakuwa wa kwa...

TMA YATOA UTABIRI WA MVUA ZA MSIMU NOVEMBA 2026 HADI APRIL 2027

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu wa Novemba 2026 hadi Aprili 2027 kwa mikoa 14 nchini, ikiwemo Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Mbeya na Ruvuma. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa mingine iliyojumuishwa katika utabiri huo ni Songea, Iringa, Njombe, Morogoro Kusini, Singida, Dodoma, Lindi na Mtwara. Utabiri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Benedict Chang'a, ukiwa sehemu ya juhudi za kuziwezesha sekta mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujiandaa na kupanga shughuli zao kulingana na matarajio ya hali ya hewa katika kipindi hicho. 7th TMA imeeleza kuwa utabiri huo wa mvua za msimu unahusu maeneo yaliyotajwa kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Novemba 2026 hadi Aprili 2027. Wakati huo huo, utabiri wa mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026 ulitolewa rasmi mwezi Agosti mwaka huu, ukihusisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kaskazini mwa Kigoma. Mikoa mingine iliyoainishwa katika utabiri...

MHE. SALOME AKUTANA NA KAMPUNI ZA CHINA KUJADILI UWEKEZAJI KATIKA MAFUTA, GESI ASILIA NA NISHATI JADIDIFU

Image
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kampuni mbili kutoka China kwa lengo la kujadili uwekezaji katika sekta ya nishati nchini, hususan katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya gesi pamoja na miradi ya nishati jadidifu. Katika kikao kilichofanyika Oktoba 23, 2026, katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, Dar es Salaam,Mhe. Salome amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ChuanQing Drilling Company, Bw. Liu Chang Xu, yaliyolenga kujadili fursa za uwekezaji katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia, ujenzi wa miundombinu katika mkondo wa chini wa sekta ya petroli pamoja na miradi ya nishati jadidifu, hususan nishati ya jua na jotoardhi. Pia, Mhe. Salome amezungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kwala Industries, Bw. Janson Huang, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Kinyerezi, Da...

DKT. HOMERA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI

Image
Dar es Salaam, Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, kuhusu maeneo mbalimbali ya ushirikiano na uwekezaji katika sekta ya nishati, hususan umeme, nishati jadidifu, mafuta na gesi asilia pamoja na nishati safi ya kupikia. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo, Oktoba 22, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam, Dkt. Homera amesema Tanzania inahitaji wawekezaji katika utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kujazia gesi asilia iliyoshindiliwa kwenye vyombo vya usafiri (CNG). Aidha, amesema Tanzania inahitaji ushirikiano wa kitaalamu na kiteknolojia katika ujenzi, uendeshaji na usimamizi wa viwanda vya kusafisha mafuta hususan wakati huu ambapo nchi ipo katika mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kusafisha mafuta mkoani Tanga. "Katika shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, tunahitaji ushirik...