SPIKA ZUNGU APOKEA JINA LA MAKAMU WA RAIS MTEULE

 


Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) leo tarehe 28 Agosti 2026 amepokea jina la Makamu wa Rais Mteule lililopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi. 


Jina hilo limewasilishwa kwa Mhe. Spika na Katibu wa Rais  Bal. Ali Jabir Mwadini akiwa ameambatana na Mpambe wa Rais (ADC) Brig. Jen. Nyamburi Mashauri kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge. 


Mapokezi ya Jina hilo yameshuhudiwa na Naibu Spika Mhe. Daniel Sillo(Mb) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari (Mb) pamoja na Katibu wa Bunge , Ndugu Baraka Leonard.




Comments

Popular posts from this blog