MAKAMU WA RAIS AIPONGEZA TPDC KWA KUCHANGISHA MIL.500 KWA AJILI YA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kukusanya Shilingi milioni 500 kupitia mbio za hisani za TPDC Marathon 2026, na hivyo kuvuka lengo la awali la Shilingi milioni 200 kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo aliposhiriki mbio za hisani za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC Marathon 2026) zilizofanyika jijini Dar es Salaam leo, tarehe 21 Novemba 2026 kwa kaulimbiu “Hatua yako, Okoa Maisha”. Fedha zilizokusanywa zitagharamia upasuaji na matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa watoto waliozaliwa na matatizo ya moyo.


















Comments
Post a Comment